Ongeza Spidi ya Computer na Ufanisi wake kwa SSD

General Description

Source: ZenjishoppazzRelease date: 2020-06-19Duty Station: Zanzibar
26152 visits!... Deadline: 2021-12-31 11:14:00

Ongeza spidi ya computer na Ufanisi wake kwa kuweka disk ya SSD

 

Kwanini kubadilisha hard disk yako kuwa SSD kutaifanya computer yako kua na speed mara 10 zaidi!!

 

Hard disk ni kifaa kinachotumika kutunza taarifa (data) katika computer au wakati mwengine katika ‘External hard disk’. Kwa kua kifaa hiki huhifadhi taarifa muhimu zinazohitajika katika utendaji wa computer na mtumiaji wa computer pia, kifaa hiki kina nafasi kubwa katika kuathiri ufanisi wa computer. 

 

Seagate 500GB SATA Laptop Hard Disk: Amazon.in: Computers ...
Hard disk ya kawaid HDD

 

 

Kuanzia mafaili ya windows, applications na mafaili binafsi ya mtumiaji, yote huhifadhiwa kwenye hard disk. Kila wakati mtumiaji anapohitaji kufanya kitendo katika computer, taarifa husomwa au kuhifadhiwa katika hard disk. 

 

Kwa nini hard disk za kawaida zinapunguza spidi ya computer?

 

Mfumo wa Diski ya Kuzunguka

Hard disk za kawaida (Hard Disk Drives) HDD zina mfumo wa disk ambayo inazunguka ili kusoma au kuweka taarifa, disk inapaswa kuzunguka ili mkono (Spindle) maalumu ambao huandika au kusoma taarifa uweze kufika mahala panapotakiwa na kufanya uandishi au usomaji wa taarifa. Kuzunguka kwa disk Kunachukua muda na pia kunatumia umeme mwingi hivyo kufanya betri kumaliza chaji haraka

 

technology drive GIF
Hard disk drive diski ya kuzunguka

 

 

Kusoma na kuweka taarifa

Taarifa huwekwa na kusomwa kwa mfumo wa smaku, pia uwezo wa disk hii kusoma na kuandika ni mdogo kwa kipimo cha sekunde. Vile vile kuna wakati disk hizi hufanya kitu kinachoitwa fragmentation, jambo hili hufanya faili moja kuhifadhiwa vipande vipande katika sehem tofauti za disk hivyo kuongeza muda wa kutafuta wakati wa kusoma faili hilo.

 

Kama Haitoshi

Hard disk hizi 

  • ni nzito hivyo huongeza uzito wa computer yako, 
  • lakini pia zikianguka ni rahisi kuharibika na kupoteza data zako. 
  • Vile vile kutokana na utendaji wake hufanya computer kupata joto (Overheat) 

 

Solid State Drive (SSD)

Buy Samsung 860 EVO 2TB SSD | Hard Drives & SSDs | Scorptec Computers
SSD Hard disk

Hizi di disk ambazo hutumia mfumo wa ki electronic kama ule wa flash disk, badala ya ule wa disk ya kuzunguka. Hivo basi utaratibu huu wa kufanya kazi huwezesha disk hii kufanya kazi kwa speed kubwa Zaidi kwa ufupi disk hizi:

 

  • Zina spidi Zaidi ya mara 10 ya hard disk za kawaida
  • Spidi za kusoma na kuandika baina ya 200MB mpaka 550MB kwa sekunde moja wakati Disk za Kawaida ni spidi baina ya 80MB mpaka 160MB kwa sekunde
  • Hutumia umeme mdogo hivyo kutunza uhai na utendaji wa betri yako
  • Ni nyepesi hivyo kuzifanya Madhubuti hata zikianguka
  • Huepusha computer kuwa slow kama vile wakati wa kuwaka au unapofungua mafaili mengi

Kama zilivyo hard disk za kawaida, hizi nazo zipo za ukubwa na makabila tofauti kama vile 128GB, 256GB, 500 GB na makabila Western Digital (WD), Seagate, Kingston na mengineyo.

 

Jinsi ya Kuzipata

Wasiliana nasi kupata disk hizi pamoja na kuwekewa windows na program kama vile Office, PDF reader, VLC media player na nyenginezo.

 

Hard disk ya zamani tutaigeuza  kuwa External Hard disk ili uweze kuhifadhi mafaili yako mengine.

 

Wasiliana nasi kwa Whatsapp +255655063601

 

 Share via Whatsapp

Promoted Ads

No preview available
Amih pure Honey (Asali mbichi)
489

Visits

TZS 13,000
No preview available
Ramani na ujenzi wa nyumba
945

Visits

TZS 300,000
No preview available
Sport fishing boat
1604

Visits

TZS 23,000,000
No preview available
Abaya baibui
2710

Visits

TZS 75,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili