Jinsi ya kupika Badia (Bagia) za Muhogo

General Description

Source: Zenjishoppazz



Release date: 2023-08-03



Duty Station: Zanzibar
8777 visits!... Deadline: 2024-02-03 22:08:00

Badia (Bagia) za Muhogo 

Badia zilizowiva Hizi ni maarufu sana haswa kule pemba, kama unapotoka ni maarufu pia tupia comment ya eneo unalotoka. 

Jinsi ya Kuandaa 

Vifaa:  

1. Muhogo mbichi kilo moja au kama unvojiskia 
2. Vitunguu maji na thomi 
3. Chumvi 
4. Pili pili (mwendo kasi)  
5. Nazi (sio lazima, ila inaongeza ladha nzuri) 

Maadalizi 
1. Menya Muhogo wako vizuri, Ukoshe  
2. Para muhogo kwa kipario (grater) 
Muhogo ulioparwa
3. Kamua muhogo ulioparwa ili kupunguza maji 
Kamua kwa kitambaa
Unga uliokamuliwa
5. Kuna nazi yako vizuri, usichanganye na maji wala usiikamue 
6. Para kitunguu maji upate vipande viduchu viduchu 
7. Vitunguu thomi vilivyotolewa magamba vitwangwe kwenye kinu na chumvi 
Tengeneza Badia Mviringo
8. Changanya muhogo ulioparwa, vitunguu, na nazi iliyokunwa kwa pamoja  
9. Hakikisha unachanganya vizuri ili chumvi na viungo vyengine ipate kuenea 
10. Kata vidonge vidogo vidogo utengeze badia kama kawaida 

Upishi 
1. Bandika karai (frying pan) weka mafuta yaache yapate moto 
Bandika mafuta
2. Ingiza badia zako, zigeuze geuze 
3. Zikiwa na rangi ya brown hapo zitakua tayari zimewiva 

Kula 
1. Mara nyingi huliwa kama snack 
2. Unaweza kula kama zilivyo au na chakne (chutney) 

Tembelea Bofya Hapa Kwa Maelezo Zaidi for more 

Badia zilizowiva  



Share via Whatsapp

Promoted Ads

No preview available
Highheels
582

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
370

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
347

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
392

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
364

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
282

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
210

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili