Kazi 4 zinazolipa mishahara mikubwa
General Description
Source: BBC Swahili
Release date: 2023-04-11
Kazi nne (4) zinazolipa mishahara mikubwa
Je wajua baadhi ya wahitimu wapya wanaanza taaluma zao kwa mishahara ambayo wafanyikazi wengi hawatawahi kufikia katika taaluma zao?
Davis Nguyen, anawasaidia waliohitimu vyuoni kuanza taaluma zao kupitia ushauri wa usimamizi. Ni tasnia ambayo kihistoria imekuwa ikilipa vizuri: hata kabla ya janga la corona, kuna baadhi ya kampuni kubwa ambazo ziliwalipa wahitimu mishahara mikubwa zaidi.
Lakini, katika soko la sasa, wateja wa Nguyen wanafanya vizuri sana. “Watarudi na kusema ‘Nina ofa mbili kuu’,” aeleza mwanzilishi huyo wa My Consulting Offer, iliyoko Georgia, Marekani. "Moja ni dola elfu 120, nyingine ni dola elfu140.
Mazingira ya leo inamaanisha wahitimu wanaweza kupata pesa nyingi zaidi kuliko miaka michache iliyopita.
Je, tunapoelekea kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya unataka kuboresha malipo yako? Zifuatazo ni taaluma ambazo unaweza kuhamia au kufanya kazi hizi.
1.Ushauri wa usimamizi
Hii ni mojawapo wa taaluma ambazo wahitimu wanazidi kwenda moja kwa moja kutoka darasani hadi katika kazi zinazolipa vizuri - kupata mshahara ambao baadhi ya watu hawatawahi kuziona maishani mwao.
Washauri wa usimamizi husaidia makampuni kutatua matatizo, kuimarisha utendaji wa biashara, kuzalisha thamani, na kuongeza ukuaji.
Kazi inayofanywa na washauri wa usimamizi inaweza kutofautiana, ambayo ni pamoja na biashara ya kielektroniki, uuzaji, usimamizi wa ugavi na mkakati wa biashara.
Kazi za kila siku za kazi ni pamoja na kufanya uchambuzi wa takwimu thabiti; mahojiano na wafanyikazi wa mteja; kuwasilisha na kuunda mapendekezo ya biashara, pamoja na kusimamia timu, kusimamia utekelezaji wa mapendekezo haya.
2.Uhandisi wa kompyuta
Siku hizi, vifaa vya kompyuta vimewekwa katika bidhaa nyingi za elektroniki, na ulimwengu umeunganishwa kupitia mifumo ya kompyuta.
Kwamujibu wa mtandao wa wa Try Engineering, kazi ya mhandisi wa kompyuta inategemea vifaa -inazingatia mifumo ya uendeshaji na programu.
Wahandisi wa kompyuta lazima waelewe muundo wa kimantiki, muundo wa mfumo wa microprocessor, usanifu wa kompyuta, upatanishi wa kompyuta, na waendelee kuzingatia mahitaji na muundo wa mfumo.
Kwa hiyo wahandisi wa kompyuta wanafanya kazi katika kila aina ya viwanda na kuendeleza na kuunganisha bidhaa na mifumo kwa njia mpya kila siku.
Katika Kampuni kubwa za teknolojia, wahandisi wa programu za kiwango cha awali mara nyingi huanza kwa mishahara mikubwa.
3.Uchambuzi wa data
Mchambuzi wa data mara nyingi kuzingatia mbinu za utafiti wa takwimu usindikaji wa data ya takwimu na uchambuzi wa matokeo ili kupata hitimisho la busara.
Katika mashirika makubwa zaidi ya benki, malipo ya wachambuzi wa mwaka wa kwanza yameongezeka kwa karibu 30% - mshahara wa msingi wa dola elfu 110 sawa na (£83,979),mara nyingine.
4. Uwakili
Wakili ni mtu ambaye alisomea sheria na kufundishwa kama mtaalamu wa sheria. Yeye ni mtaalam wa sheria na nambari za kisheria, kwa hivyo ana sifa ya kuwakilisha, kusaidia, kushauri, kutetea na kusimamia taratibu mbele ya mashirika ya umma na ya kibinafsi, kwa kuzingatia haki na masilahi ya raia ambao wanaomba huduma zake.
Katika makampuni makubwa ya sheria ya London, baadhi ya mawakili wapya waliohitimu huanza kazi zao kwa malipo ya mshahara wa pauni elfu 107,500 sawa na (dola141,115).
Nguyen anasema "vijana walioa na umri wa miaka 20 wanalipwa mshahara wa dola elfu 100,000 wameongezeka" na hiii imezidi kuwa jambo la kawaida tangu janga la corona lilipokumba ulimwengu.
Athari za muda mrefu?
Mara nyingi, wafanyakazi hawa vijana wanajiunga na makampuni ambapo wenzao walianza na malipo ya chini, na ilibidi wafanye kazi kwa bidii kwa miakakadhaa ili kupata mshahara mzuri.
Mashirika kama haya yamekuwa yakisema kuwa hatua hiyo ni jibu kwa mahitaji ya soko: mgogoro wa kukodisha unamaanisha ushindani wa vipaji unabakia kuwa mkali; ikiwa mwajiri anataka wagombea bora walio tayari kufanya kazi kwa saa nyingi, wanapaswa kuwapa malipo ya juu kufidia muda mrefu wanaofanya kazi.
Hata hivyo, zaidi ya kulinganisha kiwango cha soko, je, kuwapa wahitimu mishahara mikubwa huleta manufaa, kama vile kutoa motisha kwa saa nyingi zaidi za kaziau kuongeza maadili ya kazi? Au inaweza kuleta matokeo yasiyotarajiwa, kwa vijana wenye kipato cha juu na pia nguvu kazi kubwa?
Mishahara ya wahitimu imekuwa ikipanda kwa miaka mingi. Kulingana na data ya 2021 kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiseriklai nchini Marekani, Chama cha Kitaifa cha Vyuo na Waajiri, mshahara wa kuanzia kwa baadhi ya wafanyakazi wa ngazi ya juu katika nyanja fulani umepanda sana: kwa mfano, wastani wa mshahara wa mtaalamu wa sayansi ya kompyuta umepanda hadi dola elfu 72,173 ( £55,100) - ongezeko la 7% ndani ya mwaka mmoja tu.
Nicholas Bloom, profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Stanford, anasema mahitaji ya wafanyikazi yanazidi usambazaji wa haraka katika sekta, haswa katika teknolojia. Sekta ya fedha - yenye kazi ambazo mara nyingi zinahitaji mtu kufanya kazi kwa saa 70 kwa wiki - pia imeongeza mishahara ili kuajiri wagombeaji bora zaidi.
''Malipo ya juu hufungua fursa''
Kwa hivyo, katika hali nyingi, wahitimu wanakabidhiwa mishahara ya watu sita kama "chombo butu cha kuajiri" kati ya hali ya sasa ya soko la ajira, anaongeza Rue Dooley, mshauri wa masuala ya ajira wa Jumuiya ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (SHRM), anayeishi Marekani.
Hii inamaanisha kuwa wafanyikazi wengine wa kiwango cha juu wanaweza kupata pakiti kubwa za malipo kabla hata hawajaondoka kwenye bweni la chuo. "Tunaona mara kwa mara makampuni mara mbili kwa ukubwa kila baada ya miezi 18, kwa hivyo mishahara ya wahitimu inafuata soko kwa karibu," anaongeza Bloom.
Katika teknolojia, makampni madogo pia sasa yaanapaswa kulipa wafanyikazi wa ngazi ya juu mishahara ya juu ili kuendana na mashirika yaliyoimarishwa zaidi.
Josh Brenner, Mkurugenzi Mtendaji wa soko la walioajiriwa, mjini New York City, anasema waajiri wa Marekani wanawalipa wafanyakazi wa teknolojia wa mwaka wa kwanza wastani wa kwanza wa mshahara wa $110,027 (£84,000).
Wateja wa Nguyen ambao ndio mwanzo wamehitimu chuo mara nyingi hupata kazi na mshahara ambao ni mkubwa kuliko malipo ya jukumu lake la ushauri wa usimamizi.
Anaamini kuwa ni jambo jema. "Mishahara mikubwa kwa wafanyakazi wanaoinukia ni mwelekeo ambao ulianza miongo kadhaa iliyopita," anasema. "Malipo ya juu hufungua fursa kwa watu ambao hawangekuwa nayo, na haichukui pesa kutoka kwa wale walioanza kwa malipo ya chini."
Others
- Ajali ya MV Spice Islander
- Ifahamu Museum for the Future Dubai
- Matokeo ya Kidato cha Nne (Form Four) 2022/2023
- The Motivation Myth
- TABIA 12 ZA MATAJIRI/MAMILIONEA
- Mambo saba ya kujifunza katika kitabu cha The Richest Man in the Babylon
- History Form One Notes
- Ni yapi malengo yako kwa mwaka 2023
- MAMBO SABA WANAYOYAFANYA MASKINI, AMBAYO MATAJIRI HAWAYAFANYI
- KARIBU USAFIRI NASI KWA SAFARI YA HIJA
- NAMNA NZURI YA KUWEZA KUHIFADHI PESA