Nafasi za Kazi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ-Pemba

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2017-12-05Kituo cha Kazi/Tukio: Pemba
Imetembelewa mara! 7855 ... Deadline: 2017-12-08 00:00:00

 Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ - Pemba kama ifuatavyo:-

OFISI YA MKUU WA MKOA WA KUSINI – PEMBA:

1. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Utunzaji wa kumbukumbu) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Ustawi wa Jamii Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Ustawi wa Jamii’ (Social Work) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3. Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

OFISI YA AFISA MDHAMINI – PEMBA:

1. Afisa Manunuzi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Ununuzi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Utunzaji wa kumbukumbu) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 08 Disemba 2017 wakati wa saa za kazi. Share via Whatsapp
Advertise with us

©2023 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English