Nafasi za kazi Wizara ya mifugo maliasili na uvuvi

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2017-12-04



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 15570 ... Deadline: 2017-12-08 00:00:00

 Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi kama ifuatavyo:-

1. Microbiology (Mtaalamu wa Maabara) Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Maabara (Biotechnology and Laboratory Science) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Wildlife Tourism Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Wildlife Tourism kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3. Veterinary Medicine Daraja la II “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Udaktari wa Mifugo’ (Bachelor of Veterinary Medicine) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Agricultural Engineer Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Agricultural Engineering kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 08 Disemba 2017 wakati wa saa za kazi. 



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English