Jinsi ya kuchagua kompyuta kwa matummizi mbali mbali

Maelezo

Chanzo: Zenjishoppazz



Tarehe Iliyotolewa: 2017-10-08


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Tanzania
Imetembelewa mara! 61970 ... Deadline: 2018-10-10 00:00:00

 

KOMPYUTA INAYONIFAA

 

Zenjishoppazz imekuandalia makala itakayo kusaidia katika mchakato mzima wa kuchagua kompyuta kwa ajili ya matumizi mbali mbali.

 

Kwa kuzingatia kwamba muda umewadia wa wanafunzi kuingia katika vyuo mbali mbali nchini. Wakiwa katika maandalizi huingia katika wakati mgumu wa kuchagua ni aina gani ya kompyuta itawafaa Zaidi na wataweza kuinunua. Tafadhali endelea kusoma ili upate majibu kwa ufupi.

 

1.    Aina za watumiaji

 

a.    Watumiaji wa kawaida. (Group 1)

 

Hawa hawategemei sana power ya kompyuta kutokana na matumizi yao kua mepesi kama vile kuandaa na kuprint Makala kwa kutumia Microsoft word, Excell au power point. Pia hutumia kwa ajili ya kuperuzi mtandaoni, ku play mafaili ya sauti au video na kuangalia picha. Mfano wa watumiaji hawa ni Makarani wa Ofisini, Wanafunzi wa Arts na Sayansi jamii, Wanafunzi wa masomo ya Biashara, Watumiaji wa nyumbani na wenye maduka.

 

 

 

b.    Watumiaji maalumu (Group 2)

 

Hawa huwa na matumizi mazito ambayo yanahitaji rasilimali nyingi za kompyuta kama vile uwezo wa processor, ukubwa wa RAM na uwezo wa display wa kompyuta. Mfano wa watumiaji hawa ni Architecture students, wanafunzi wa Computer, Telecom na kozi nyengine za Engineering , Graphic designers, wanaofanya Video and Image processing na Gamers.

 

2.   Vigezo:

 

Vigezo vikubwa vinavyoangaliwa katika kompyuta ni Uwezo wa processor, RAM na uwezo wa kuhifadhi yaani ukubwa wa Hard disk. Hapa tutaangalia kwa ufupi vigezo hivi kama ifuatavyo.

 

Image loading

 

Figure 1 kompyuta na specification zake

 

 

 

 

 

a.    Uwezo na ufanisi wa computer (Power and Performance)

 

Vitu vinavyopelekea ufanisi mzuri wa kompyuta

 

i.        Processor:

 

a.     Huu ndio ubongo wa kompyuta, hupimwa kwa mizunguko ya utendaji (Processing Cycles) ambazo hutajwa kwa kipimo cha Giga Hartz mara nyingi. Mfano processor yenye ukubwa wa 1 GHz ina uwezo wa kufanya vitendo Bilioni moja ndani ya sekunde moja

 

 

 

b.    Zilizo maarufu sokoni kwa sasa za kampuni ya Intel ni dual core, Core i3, Core i5 na Core i7, zipo pia za kampuni ya AMD lakini hizi si maarufu sana na zinaweza kuwa changamoto kwa watumiaji hasa wa group 2, hizi huwa na kasi (Speed) Zaidi na processing cycles nyingi Zaidi kila namba ya core inavyoongezeka. Hata hivyo bei nayo huongezeka.

 

 

 

c.     KILA PROCESSOR INAVYOKUA KUBWA NDIVYO SPIDI YA KOMPYUTA INAVYOONGEZEKA

 

 

 

ii.        RAM

 

a.    Ni memori ya kuhifadhia mafaili yanayotumika kwa muda na baadae hufutwa, hii huwepesisha upatikanaji wa mafaili na hivyo kuifanya kompyuta iwe na kasi (Speed) Zaidi kila ukubwa wa RAM unavyoongezeka.

 

b.    RAM kama memory card za simu, hupimwa kwa GB, zipo RAM za 1GB, 2GB, 4GB, 16GB na kuendelea.

 

c.    KILA MEMORY INAPOKUA KUBWA NDIVYO SPIDI YA KOMPYUTA INAKUA KUBWA.

 

iii.        Graphics (Display)

 

a.    Hii inawahusu sana watumiaji wa group 2 ambao hufanya kazi kama za Architectural drawing, Gaming, Adobe photoshops, Image na video processing. Zipo za Intel za ukubwa kama vile 2GB au 4GB.

 

b.    Ambazo ni maarufu sana ni za NVIDIA ambazo hujulikana kwa jina la NVIDIA graphics kama vile NVIDIA GFORCE,  kuanzia NVIDIA 700 na kuendelea hufanya vizuri zaisi.

 

c.     Ukubwa wa screen hutegemea na chaguo la mtu. Laptop hupatikana kama mini, inch 13, 14, 16 na 17.

 

 

 

Maoni yetu:

 

·         Wengi wa watumiaji wa group 1 wanaweza kukamilisha kazi zao vizuri kwa kompyuta yenye uwezo wa Pentium Processor, 2GB RAM na 500GB

 

 

 

·         Kompyuta yenye processor Intel Core i3, RAM 4GB, hard disk 500GB na Intel graphics za kawaida inaweza kufaa kwa watumiaji wote wa group 1 na wengi wa group 2 katika mazingira ya kitanzania.

 

 

 

Unaweza kuangalia vitu hivi kwenye kompyuta kwa kubonyeza

 

Right click My computer (or This PC kwenye window 8 na 10)

 

Image loading


 

halaf bonyeza kwenye properties utaweza kupata screen kama hii


 

Image loading

 

 

 

b.    Uhifadhi (Hard disk)

 

i.    Ukubwa:

 

·         Ukubwa huangaliwa kwa kutazama Gigabytes ambazo kompyuta inaweza kuhifadhi zilizo maarufu ni 250GB, 320GB, 500GB, 750GB na 1 Tera Byte (1000GB). Kwa wastani 500GB ni nzuri kwa matumizi na bei pia ni nzuri ukilinganisha na zenye ukubwa Zaidi ya hapo.

 

 

 

·         Hard disk ya SSD hua ghali Zaidi na hivyo kuifanya kompyuta kua ghali ukilinganisha na hard disk yenye ukubwa sawa ya HDD

 

ii.    Aina:  

 

Hard Disk Drive(HDD) au Solid-State Drives (SSD)

 

1.    Aina ya kwanza ambayo ndiyo ya zamani ni HDD, hii hua na disk ambayo inazunguka ndani yake wakati wa kuchukua au kuweka data. Aina hii huchangia kwa kiasi Fulani kupunguza kasi(Speed) ya kompyuta kutokana na muda unaochukuliwa kusoma au kuweka data ndani yake.

 

 

 

2.    Aina ya pili ambayo nidyo ya kisasa Zaidi ni Solid State Drive ambayo teknolojia yake hufanana na ile ya flash disk au RAM yaani haina mfumo wa disk ndani yake. Hii huzifanya disk hizi kua na speed na umadhubuti Zaidi. Lakin kutokana utengenezwaji wake hua na bei ya juu na hufanya kompyuta kuongezeka bei.

 

 

 

 

 

b.    Aina ya Kompyuta (Brand)

 

Katika top 5 ya kompyuta za laptop duniani huwezi kuikosa dell, Hp na Apple zikiwemo na Lenovo na Asus. Kwa mtazamo wetu hii hapa ni ranking yetu kwa kulinganisha Kudumu(Uzima), Bei na Ufanisi wa kazi.

 

 

 

S/NO

JINA LA BRAND

MAELEZO

1

Dell

Hudumu sana, betri inatunza chaji wastani, ufanisi mzuri, matatizo ya adapter

2

Acer

Bei rahisi kwa ufanisi mkubwa, hudumu sana, betri inatunza chaji wastani.

3

Toshiba

Bei nzuri, ufanisi, chaji wastani matatizo ya screen

4

Hp

Bei ya juu kidogo (Mpya), utendaji mzuri, hudumu sana, matatizo ya Joto (overheat)

5

Apple (Macbook)

Hudumu sana, utendaji mzuri, betri hutunza chaji vizuri. Bei ya juu kiasi.

 

 

 

c.    Uzima (Durability)

 

Hii inategemea na mtumiaji kwa kiasi Fulani lakini pia aina ya kompyuta huchangia kudumu au kutokudumu kwa kompyuta kama ilivyoonekana hapo juu, kwa uzoefu wetu kompyuta za dell zimeonesha kua ni zenye kudumu Zaidi zikifuatiwa na Acer, Hp na Toshiba.

 

d.    Bei (Price)

 

Bei huchangiwa na vitu tulivyovitaja hapo juu kama ifuatavyo:-

 

i.    Ufanisi: Bei ya kompyuta hutegemea sana ufanisi wake yaani vitu vinavyopelekea ufanisi wa kompyuta. Kila RAM na Processor zinavyokua kubwa ndivyo bei ya kompyuta inavyoongezeka, uwezo wa kuhifadhi yaani (Storage) pia huchangia kuongeza bei.

 

 

 

ii.    Aina ya kompyuta: Brand(Majina) ya kompyuta pia yanafanya bei kutofautiana hata kama yatakua na ufanisi sawa. Kwa kawaida kompyuta kama za Hp, Dell na Macintosh zina bei ya juu ukilinganisha na Toshiba, Asus, Samsung or Lenovo na kwa kiasi Fulani hii huonesha pia ubora na uzoefu wa kampuni hizo katika utengenezaji wa kompyuta hizo.

 

Maoni Yetu:

 

iii.    Kwa ushauri Kompyuta za Acer hua na ufanisi nzuri, hudumu na bei ya wastan hasa kwa wale ambao ni watumiaji wa group 2. Ikifuatiwa na dell na Toshiba na Hp.

 

iv.    Kuanzia wastani wa fedha za kitanzania 400,000 na kuendelea unaweza kujipatia kompyuta nzuri iliyotumika (used) na hata mpya.

 

 

 

 

 

e.    Used, Refubrished au Mpya?

 

Hii hutegemea Zaidi na uwezo wa kifedha wa mtu. Kwa sasa zipo kompyuta nyingi mpya zenye bei nzuri hususan kwa watumizi wa Group 1. Kwa watumiaji wa Group 2 kompyuta mpya hua na bei Zaidi. Hata hivyo ikiwezekana inashauriwa kununua kompyuta mpya ili kuepusha usumbufu na gharama zinazoweza kujitokeza kutengenza kompyuta zilizotumika.

 

Used:

 

Kompyuta kama vifaa vyengine hutengenezwa na lifespan yake (Yaani Umri unaotegemewa) hivyo basi kompyuta used huwa tayari zimeshatumia muda wake na hili hufanya ununuzi wake kua wa kubahatisha kwa kiwango Fulani.

 

 

 

Kwa kuzingatia vigezo tulivyovitaja hapo juu unaweza kupata kompyuta nzuri tu ya used kwa bei nafuu ambayo bei ya mpya yenye uwezo huo huwa mara mbili au Zaidi.

 

                   Refubrished:

 

Hizi ni kompyuta ambazo zimetumika na kurejeshwa kiwandani au kwa authorized maintenance dealers wa kampuni husika na baadae kuingizwa tena sokoni. Ni vizuri kuwa makini kwani wakati mwengine kompyuta hizi huuzwa kama mpya. Mara nyingi huekewa label (karatasi) inayoonesha kua kompyuta hii ni Refubrished.

 

f.     Venginevyo

 

i.    Operating system: kwa kawaida Windows ndio maarufu na rahisi kutumia kwa watu wengi, hiii inauzwa japo hupatikana kwa mafundi kwa be ya chini kuliko ile halisi. Zipo linux operating systems kama Ubuntu, Linux Mint na nyenginezo ambazo kwa pamoja hujulikana kama Ubuntu, hizi ni za bure yaani (Open source ). Zipo pia za Apple ambazo huja na kompyuta zenyewe.

 

ii.    Kati ya 64bit na 32 bit Windows ni vizuri kuchagua 64 bit, hii huwezesha kompyuta kutumia vizuri RAM iliyopo na huongeza spidi pia.

 

iii.    Kwa sasa Windows 10 ndio mpya Zaidi na inapendekezwa,  ipo Windows 8 na 7

 

 

 

Tafadhali wasilisha maoni yako hapa chini au tuma kupitia email: info.zenjishoppazz@gmail.com

 

Tags: Jinsi ya kuchagua computer, Vitu vya kuzingatia wakati wa kuchagua kompyuta, How to choose the right pc, things to consider when buying computer

 

 

  



Download

Share via Whatsapp

Bidhaa Mbalimbali

Zenye Promotion

No preview available
Highheels
296

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
237

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
200

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
227

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
221

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
140

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
102

Visits

TZS 3,000
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English