Mambo Ambayo Yanaweza Kukupotezea Muda ikiwa utayafanya.

Maelezo

Chanzo: ZenjishoppazzTarehe Iliyotolewa: 2023-05-25Kituo cha Kazi/Tukio: TANZANIA
Imetembelewa mara! 11934 ... Deadline: 2024-07-25 01:03:00

Mambo Ambayo Yanaweza Kukupotezea Muda ikiwa utayafanya.

 

  1. Kujaribu kumfurahisha kila mtu.
  2. Kufikiri kupita kiasi
  3. Kurudia kufanya makosa yale yale.

Jambo ambalo linawapotezea muda watu wengi ni kujaribu kutaka kumfurahisha kila mtu (kitu ambacho hakiwezekani), pasi na kujali muda na kipaumbele ulichokipanga kukifanya katika muda husika. Kwa mfano ili kuweza kufanikiwa unatakiwa ujifunze 

• kusema hapana katika baadhi ya mambo

• Tanguliza mahitaji yako mwenyewe yale ambayo tayari umeshayapanga

•Tafuta mahusiano kwa kusaidiana na kushauriana na wengine

 

Kufikiri kupita kiasi ni jambo lililowasababishia watu wengi matatizo kama vile stress na kuwapotezea watu muda. Ili kuweza kulishinda jambo la kufikiri kupita kiasi fanya mambo yafuatayo

• Andika mawazo yako

• Fanya mazoezi mara kwa mara.

•Tumia maongezi mazuri ya kibinafsi baina yako na wengine

 

Unapojaribu kufanya makosa yale kwa yale ni katika jambo linaloweza kukurejesha nyumba kimaendeo. Hivyo ili kuondokana na tatizo hilo fanya mambo yafuatayo

• Jipange upya ili kuepuka makosa yale yale

• Tafuta maoni kutoka kwa watu tofauti ili uweze kuyaepuka kurejea tena

• Tafakari juu ya kosa ulilolifanya nyumba ili usilirejee tena.Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English