Mambo saba ya kujifunza katika kitabu cha The Richest Man in the Babylon

Maelezo

Chanzo: Zenjishoppazz



Tarehe Iliyotolewa: 2023-01-17


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: TANZANIA
Imetembelewa mara! 18341 ... Deadline: 2025-03-17 00:00:00

MAMBO SABA (7) UNAYOWEZA KUJIFUNZA KAMA UTASOMA KITABU “RICHEST MAN IN BABYLON”

Kama ni msomaji na mfuatiliaji mzuri wa vitabu hasa vinavyozungumzia masuala ya ujasiria mali na stadi za Maisha, basi tambua kuna vitabu tofauti tofauti ni muhimu vya kusma ambavyo vitakusaidia katika safari yako, miongoni mwa vitabu hivyo ni Richest Man in Babylon ambacho kinaweza kukufundisha mambo mengi. Hivyo tambua mambo saba (7) muhimu ambayo unaweza kujifunza kupitia kitabu chichi.

  1. Jilipe wewe mwenyewe asilimia 10% ya kipato chako. Hii itakusababishia kurekebisha bajeti yako ili kuendana na uwezo wako ndani ya asilimia 90% iliyobakia. Jambo hili litakufanya uweze kupiga hatua kubwa sana ya kimaendeo.
  2. kuepuka matumizi yasio ya lazima kwa kuyadhibiti matamanio. Mara nyingi matamanio na shauku huja huja wakati utapopatikana mwanya wa kuyatekeleza matamanio hayo. Zisome tabia zako kwa kuepuka matumizi yoyote yasiyo ya lazimakwa kuzivuruga pesa,
  3. Acha pesa ifanye kazi kwa ajili yako kwa kukiwekeza kila unachokipata katika akiba. Hakikisha unawekeza kila faida unayoipata ili kufanya utajiri wako unaengezeka kwa haraka sana.
  4. Jaribu kuwekeza katika uwekezaji ambao utakuwa ni salama kwako wewe kwa ajili ya kuziepusha pesa zako na uharibifu na kupotea. Hakikisha unajitahidi kadiri ya uwezo wako wako ili kuhakikisha pesa zako hazipotei ovyo.
  5. Miliki nyumba yako mwenyewe kadri inavyowezekana kama itakusaidia katika ukodishaji. Ikiwa utaweza kukodisha vyumba katika nyumba yako kwa ajili ya kupunguza matumizi yako, basi fanya hivyo itakusaidia katika Maisha yako kwa kuinua kipato chako.
  6. Kuna siku ambazo utakuwa huwezi kufanya kazi kutokana na uzee, au hata kuingiza pesa. Hivyo jitayarishe kisaikolojia na kimaisha kwa ajli ya kustaafu ili usije ukapata tabu ya kutafuta pesa katika utu uzima.kujitayarisha mapema mapema ndipo utakapokuja kupata mafanikio Zaidi utu uzimani.
  7. Engeza uwezo wako wa kupata pesa Zaidi kwa kukusanya ujuzi Zaidi. Kwa hakika ni ngumu kwa kila mmoja wetu kupata ujasiri ambao utapelekea kuweza kufanikiwa katika hamu na malengo yake ya Maisha ya baadae.

Kama unataka kusoma kitabu hichi au kupakua ni bure kabisha kwa kubonyeza neno download hapo juu.



Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English