Wito usaili Wizara ya Fedha na Mipango
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2018-04-11

Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia wale wote walioomba nafasi za kazi Wizara ya Fedha na Mipango - Pemba na ambao walifanya usaili wa awali tarehe 26/03/2018 kwamba wafike Skuli ya Fidel Kasro - Pemba kwa ajili ya kufanya usaili wa mara ya Pili kwa utaratibu ufuatao hapo chini:-
Wasailiwa wote wanatakiwa wachukue vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, Cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
MCHANGANUO WA USAILI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO PEMBA
NAM. TAREHE NAFASI YA KAZI
1. 14/4/2018 MKAGUZI WA NDANI DARAJA LAII
2. 15/4/2018 MHASIBU DARAJA LA II
3. 16/4/2018 MSAIDIZI MHASIBU DARAJA LAIII
KARANI MAPATO DARAJA LA III
4. 17/4/2018 MHAKIKIMALI DARAJA LA II
5. 18/4/2018 MHAKIKIMALI MSAIDIZI DARAJA LA III
AFISA UTUMISHI MSAIDIZI DARAJA LA III
Mahala pa usaili wote huo utafanyika katika Skuli ya FIDEL KASRO PEMBA.

Zinazofanana
Bidhaa Mbalimbali
Zenye Promotion
Bidhaa Nyenginezo
Tembelea pia
