Nafasi za kazi ofisi ya tume ya mipango Zanzibar
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 0000-00-00
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Tume ya Mipango Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-
1.Dereva Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Udereva na awe na leseni hai ya udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2.Afisa Manunuzi na Ugavi Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Manunuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
3.Mhudumu Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.
4.Mpiga Chapa Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5.Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Daraja la II “Nafasi 4” Unguja
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ufuatiliaji na Tathmnini kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
6.Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 6” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7.Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 4” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
8.Afisa IT Daraja la II “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya IT kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
9.Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
10.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.
11.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2018 wakati wa saa za kazi.
Who's Online
Hits 41252 | 46 online
Announcements
- 1. TANGAZO ZA NAFASI ZA KAZI KATIKA OFISI YA TUME YA MIPANGO ZANZIBAR
- 2. TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
©2018 President's Office Constitution, Legal Affairs, Public Service and Good Governa