Nafasi za Kazi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
Maelezo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/L/116 21 Mei, 2021
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi (10) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.0 MWAJIRI: OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI (NAOT) 1.0.1 MKAGUZI DARAJA LA II - (NAFASI 10)
1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua nyaraka za matumizi, maendeleo, amana, wakala, mifuko, miradi maalum na mapato ya Serikali;
- Kushiriki kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa kazi wa ukaguzi kila mwaka;
- Kushiriki kufanya tathmini ya mpango wa kazi na kupendekeza mabadiliko inapobidi kulingana na tathmini ya taarifa ya utekelezaji ya mpango wa kazi;
- Kuhakikisha kuwa hoja na barua za ukaguzi zinatolewa na kushughulikiwa kwa wakati unaotakiwa;
- Kushiriki kutayarisha na kutekeleza mpango wa ukaguzi (Audit Programme;
- Kushiriki kupanga na kuratibu mpango wa kazi za ukaguzi;
- Kutayarisha hoja na barua za ukaguzi; na
- Kutunza daftari za kumbukumbu mbalimbali za hesabu katika kituo chake kwa maelekezo ya kiongozi mahali pa kazi