Kuomba Paspoti Mtandaoni-Uhamiaji

Maelezo

Chanzo: Uhamiaji



Tarehe Iliyotolewa: 2017-10-20


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Tanzania
Imetembelewa mara! 15596 ... Deadline: 2018-10-25 00:00:00

 

IDARA YA UHAMIAJI

 

TANGAZO KWA UMMA:

 

IDARA YA UHAMIAJI ZANZIBAR, INAWATAARIFU KWAMBA IMEANZISHA HUDUMA YA KUJAZA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI KUPITIA TOVUTI YAKE; www.immigration.go.tz. HII NI HUDUMA MPYA INAYOMUWEZESHA MUOMBAJI KUJAZA FOMU HIYO POPOTE

 

ALIPO.

 

MUOMBAJI BAADA YA KUJAZA FOMU HIYO NA KUAMBATISHA PICHA YAKE KAMA ATAKAVYOELEKEZWA MTANDAONI, ATATAKIWA KUICHAPISHA (PRINT) FOMU HIYO NA KUIWASILISHA KATIKA OFISI YA UHAMIAJI ILIYOPO KARIBU NAYE PAMOJA NA VIELELEZO HUSIKA, KWA MUJIBU WA

 

MADHUMUNI                    YA                    SAFARI                   YAKE.   

 

 

 

MADHUMUNI YA HUDUMA HII, KUONDOA USUMBUFU KWA MTEJA

 

KWENDA OFISI ZA UHAMIAJI KUCHUKUA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI NA PIA ITAMUWEZESHA MTEJA KUFUATILIA HATUA LILIPOFIKIA OMBI LAKE, KWA NJIA YA MTANDAO. AIDHA HUDUMA HII HUSAIDIA KATIKA KUIMARISHA UTUNZAJI WA TAARIFA ZA MWOMBAJI KIELEKTRONIKI.

 

HIVYO, KUANZIA TAREHE YA TANGAZO HILI IDARA, INAWATAKA WAOMBAJI WOTE WA HUDUMA YA PASIPOTI ZANZIBAR, KUJAZA FOMU ZA MAOMBI KWA NJIA HIYO YA KIELEKTRONIKI.

 

IMETOLEWA NA;  KITENGO CHA UHUSIANO, AFISI KUU YA UHAMIAJI, ZANZIBAR.

 

18 OKTOBA, 2017.

  



Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2025 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English